Uko hapa: NyumbaniMichezoNdondi2021 12 26Article 581218

Boxing News of Sunday, 26 December 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Seleman Kidunda achafuliwa rekodi na Mkongo

Pambano la Kidunda na Katompa limemalizika kwa sare katika raundi ya tatu Pambano la Kidunda na Katompa limemalizika kwa sare katika raundi ya tatu

Pambano la Selemani Kidunda dhidi ya Tshimanga Katompa limeishia raundi ya tatu na matokeo ni droo.

Pambano hili la raundi 10, la kugombea mkanda wa WBF limeishia raundi ya tatu baada ya Katompa kumfanyia faulo Kidunda iliyomfanya kupasuka juu ya jicho lake la kulia na pambano kusimama.

Kwa sheria za WBF kama pambano lingefikia raundi ya nne basi lingempa faida zaidi Selemani Kidunda lakn kwa kuwa halijafikia raundi ya nne, lilimalizika kwa sare.

Seleman Kidunda kabla ya Pambano lake la usiku wa leo alikua amecheza mapambano saba ya ngumi za kulipwa na kushinda yote kwa KO.

Hivyo kwa mara ya kwanza amepata sare katika maisha yake ya ubondia wa ngu,mi za kulipwa.