Uko hapa: NyumbaniMichezoNdondi2021 11 22Article 573478

Boxing News of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Shalom : Adam Azim atakuwa bondia bora Uingereza

Adam Azim atabiriwa makubwa katika masumbwi Adam Azim atabiriwa makubwa katika masumbwi

Wakala wa bondia kinda wa Uingereza, Adam Azim, Ben Shalom amesema bondia huyo atakua bondia bora wa Uingereza hapo baadae kutokana na kipaji alichonacho.

“Adam Azim anaenda kuwa Superstar na tupo hapa kwajili ya kushuhudia hilo”, alisema wakala Ben Shalom baada ya ushindi wa kushangaza katika pambano lake la Jumamosi.

“Tumekuwa tukiongea kuhusu Adam kwa muda mrefu. hiyo inaonyesha ni jinsi gani kijana huyu ametengenezwa.

“Nadhani tuna staa wa kipekee mikononi mwetu. Nadhani huu ni mwanzo wa kitu. Huu utakua usiku ambao watu wataukumbuka baada ya miaka kadhaa na kusema, nilikuwa pale.” aliongeza Shalom.

Adam, 19 alionyesha spidi ya hali ya juu katika raundi ya pili ya pamabano lake na Stu Greener na kupata ushindi kabla ya kusherekea ushindi na mashabiki katika uwanja wa SSE Arena, Wembley Jumamosi usiku.