Uko hapa: NyumbaniMichezoNdondi2021 10 12Article 562783

Boxing News of Tuesday, 12 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Twaha Kiduku amtaka mbabe wa Dullah

Bondia Twaha Kiduku Bondia Twaha Kiduku

Usiku wa Oktoba 9, bondia Matanzania Abdallah Pazi maarufu kama "Dullah Mbabe" katika ukimbi wa PTA, alipanda ulingoni kuzichapa na bondia kutoka DR. Congo Tshimanga Katompa.

Bondia Tshimanga Katompa aliibuka mshindi kwa kumchapa, Dulla Mbabe kwa pointi kwenye pambano la raundi 10, lakini katika moja ya kauli zake alimtaka bondia mwingine kutoka nchini Twaha Kiduku.

Sasa Twaha Kiduku ameibuka na kusema anamtaka bondia huyo wakati wowote ambao yeye atakua tayari.

"Yeye ndio amesema ananitaka lakini nimwambie tu niko tayari, muda wowote atakaojisikia mi bondia na kazi yangu ni kupigana" amesema Kiduku