Uko hapa: NyumbaniBiashara2022 01 07Article 583891

Habari za Biashara of Friday, 7 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Airtel Africa Kuzipiga Mnada Mali za Airtel Tanzania

Airtel Africa Kuzipiga Mnada Mali za Airtel Tanzania Airtel Africa Kuzipiga Mnada Mali za Airtel Tanzania

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Africa imetangaza kuwa imeanza mchakato wa kuuza mali zake za minara ya mawasiliano nchini Tanzania kwa ubia (JV) unaojumuisha wamiliki/waendeshaji wawili wa miundombinu ya mawasiliano duniani.

Kwa mujibu wa taarifa za Business Insider, JV inamilikiwa na kampuni tanzu ya SBA Communications Corporation, pamoja na Paradigm Infrastructure Limited yenye makao yake makuu nchini Uingereza ambayo inamiliki hisa chache.

Taarifa ya Airtel Africa pia imeeleza kuwa gharama ya jumla ya muamala huo ni dola milioni 176.1. zaidi ya Tsh. Bilioni 406.2. Tayari, JV imeilipa Airtel Africa takriban Tsh. Bilioni 366 na hii inafuatia kukamilika kwa awamu ya kwanza ya shughuli hiyo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kuwa salio lililosalia litalipwa kwa awamu baada ya minara iliyosalia kuhamishiwa kwenye kampuni ya JV.

Pia, Airtel Africa ilifikia makubaliano na mnunuzi ili kuwezesha kampuni yake tanzu ya Airtel Tanzania "kuendelea kuendeleza, kutunza na kuendesha vifaa vyake kwenye minara chini ya mipango tofauti ya ukodishaji, inayofanywa kwa kiasi kikubwa kwa fedha za ndani, na Mnunuzi."

Kumbuka kuwa Airtel Africa ingetenga kiasi Tsh. Bilioni 138 (zikiwa ni mapato kutokana na shughuli hiyo) kwa ajili ya kuboresha mtandao wake na miundombinu ya mauzo katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Sehemu ya Tsh. Bilioni 138 pia zingegawiwa kwa Serikali ya Tanzania ambayo inamiliki 49% ya hisa za kampuni hiyo. Wakati huo huo, salio lililosalia kutokana na muamala huo litatumika kulipia baadhi ya madeni ya Airtel Africa Group.