Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 10 12Article 562858

Habari za Biashara of Tuesday, 12 October 2021

Chanzo: ippmedia.com

BOA kuimarisha zaidi huduma zake

BOA kuimarisha zaidi huduma zake BOA kuimarisha zaidi huduma zake

Akizungumza katika kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Mkurugenzi Mtendaji wa BOA Africa, Adam Mihayo, alisema:

“Huduma kwa wateja inabaki kuwa eneo kuu la kuzingatia katika shughuli zetu za kila siku kama benki kupitia kauli mbiu yetu ya mwaka huu ya ‘Nguvu ya Huduma’, benki imeanza kufanya maboresho zaidi ambayo yatanufaisha wateja sambamba na kufanikisha kuleta maendeleo ya nchi.”

Alisema hivi sasa wateja wanaendelea kufurahia huduma za benki kupitia matawi yake yaliyopo mikoa mbalimbali nchini na njia nyinginezo mbadala za utumiaji teknolojia ya kidigitali kupata huduma za kibenki ikiwamo matumizi ya mifumo ya BOA Pay inayowawezesha wateja kufanya malipo na makusanyo wakiwa katika maeneo yao ya kazi au wakiwa nyumbani.

Mapema mwaka huu Bank of Africa iliwekwa kuwa miongoni mwa benki 15 zinazoongoza barani Afrika, ikiwa na mtaji wa dola bilioni 2.5, “Tunaamin hatua hii kubwa isingeweza kutimizwa bila wateja wetu, hivyo tunaahidi kuendelea kuwahudumia kwa bidi, hii ikiwa kipaumbele cha msingi katika biashara yetu,” alisema Mihayo.