Uko hapa: NyumbaniBiashara2022 01 12Article 585199

Habari za Biashara of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Balsingh Bosi Mpya Airtel

Balsingh Bosi Mpya Airtel Balsingh Bosi Mpya Airtel

KAMPUNI ya Airtel Tanzania Plc imetangaza mabadiliko katika timu yake ya uongozi kwa kumteua Dinesh Balsingh kuwa Mkurugenzi Mkuu Mteule wa Airtel Tanzania Plc, kufuatia kujiuzulu kwa George Mathen. Taarifa iliyotolewa Jumatano na Airtel, imesema Balsingh ataanza kazi kuanzia Januari 2022.

Balsingh ni mtaalamu wa Mauzo na Masoko aliye na uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika tasnia ya Mawasiliano ya Simu, akiwa amefanya kazi katika uwanda na majukumu mengi. Ameongoza kazi mbalimbali kama vile Mauzo, Masoko na Huduma kwa Wateja wakati wa kazi yake na ana uzoefu mkubwa wa uongozi wa kusimamia shughuli katika nchini za India na Nigeria.

Balsingh alianza taaluma yake na kampuni ya Hutchison Essar Ltd mwaka wa 2000. Baadaye alihamia Airtel mwaka wa 2006 na Tata Docomo mwaka wa 2011.

Baadaye, alijiunga tena na Airtel nchini Nigeria ambako hivi majuzi, alikuza ukuaji wa hisa katika nafasi yake kama Afisa Mkuu wa Biashara. Balsingh ana Shahada ya Uzamili katika Utawala wa Biashara kutoka Shule ya Usimamizi ya Thiagarajar.