Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 10 13Article 562933

Habari za Biashara of Wednesday, 13 October 2021

Chanzo: Mwananchi

Bei mpya za kuunganisha maji kutangazwa hivi karibuni

Bei mpya za kuunganisha maji kutangazwa hivi karibuni Bei mpya za kuunganisha maji kutangazwa hivi karibuni

Baada ya kuwepo kwa malalamiko ya gharama tofauti za uanganishwaji maji, hatimaye Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) inatarajia kutangaza bei elekezi kwa wateja.

Hayo yameelezwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja katika hafla ya kukabidhi mifano ya hundi kwa wananchi wanaopisha ujenzi wa mradi wa maji Mshikamano, Mbezi Makabe jijini humo.

Oktoba 3 mwaka huu katika hafla ya utilianaji saini utekelezaji wa mradi wa maji Mshikamano Waziri wa Maji, Jumaa Aweso aliyekuwa mgeni rasmi, aliwaagiza Dawasa kuwa na muongozo mahususi wa kuanganishiwa maji.

“Leo ukiangalia REA (Wakala wa Nishati Vijijini) umeme kuunganishwa ni Sh27,000 lazma Wizara na Mamlaka zetu za maji mje na muongozo mahususi wa gharama za kuunganishiwa maji ni kiasi gani,” aliagiza.

Akizungumzia hatua walizochukua kuhusu maagizo hayo, Ofisa Mtendaji huyo amesema tayari suala hilo limeshafanyiwa kazi na bodi inatarajia kutangaza gharama hizo muda wowote kuanzia sasa.

“Tumeshafanyia kazi kuhusu suala la gharama za utumiaji maji majumbani,na bodi siku yoyote itatangaza hilo,” amesema Luhemeja.

Wakati kuhusu fidia kwa wakazi wanaopisha mradi huo wa mshikamano, amesema wananchi saba wamelipwa kupisha ujenzi huo ambapo Sh 232.6 milioni zimetumika.

Mradi huo wenye thamani ya Sh5.4 bilioni unatarajiwa ujenzi wake kuanza mwezi huu na kukamilika Oktoba mwakani.