Uko hapa: NyumbaniBiashara2022 01 11Article 584830

Habari za Biashara of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Bei ya mafuta duniani yaongezeka kufuatia machafuko Kazakhstan

Bei ya mafuta duniani yaongezeka kufuatia machafuko Kazakhstan Bei ya mafuta duniani yaongezeka kufuatia machafuko Kazakhstan

Machafuko katika nchi ambayo ni mwanachama wa kundi la Opec+ ya Kazakhstan yamesabisha bei ya mafuta kuongezeka wakati wawekezaji wakikhofia kukatizwa kwa shughuli ya usambazaji bidhaa hiyo.

Hata hivyo soko la madini ya Urani linaonesha kutoathirika licha ya nchi hiyo ya Asia ya Kati kuwa mzalishaji wa pili mkubwa wa madini hayo duniani.

Maandamano yameenea katika nchi hiyo ya watu milioni 19 wiki hii yakisababishwa na hasira iliyochochewa na ongezeko la bei ya mafuta ya petroli. Rais Kassym-Jomart Tokayev wa Kazakhstan amesema utulivu umerudi katika nchi hiyo baada ya siku kadhaa za machafuko ambayo yamesababisha watu 150 kuuwawa.

Aidha rais huyo ameuambia muungano wa kiusalama wa kikanda unaoongozwa na Urusi kwamba operesheni ya kupambana na aliowaita ‘magaidi’ itakamilishwa hivi karibuni na kwamba kilichofanyika nchini humo ni jaribio la mapinduzi lililofanywa na watu waliotaka kuchukua madaraka.