Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 10 12Article 562816

Habari za Biashara of Tuesday, 12 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Boss Samsung hatiani matumizi ya dawa za usingizi

Jae Yong, Mwenyekiti wa Samsung Jae Yong, Mwenyekiti wa Samsung

Mwenyekiti wa kampuni ya kutengeneza simu aina ya Samsung, Korea Kusini , Lee Jae Yong, amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kutumia dawa za usingizi zinazotumika wakati wa upasuaji kinyume na taratibu za kitabibu.

Kiongozi huyo ambaye ni tajiri wa 297 duniani kwa mujibu wa Forbes, ana shutumia kutumia dawa hizo mara kwa mara katika kliniki moja ya upasuaji bandia iliyopo Seoul kati ya mwaka 2017 na 2018.

Dawa hizo ambazo kitaalamu zinaitwa 'anaesthetic propofol' hutumiwa na baadhi ya watu kama sehemu ya kiburudisho na matumizi ya dawa yanatajwa kama moja ya sababu zilizosababishwa kifo cha nyota wa muziki wa miondoko ya 'pop' Michael Jackson mwaka 2009.

Matumizi ya dawa hizi huonekana kama kosa dogo nchini humo na baadhi ya waendesha mashtaka nchini humo walipendekeza kiongozi huyo kutozwa faini ya milioni 50 mara ya kwanza kushtakiwa kwa matumizi hayo.

Jambo ambalo lilipingwa na Mahakama na kuamuru kusikilizwa rasmi kwa shauri hilo,