Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 11 16Article 571783

Habari za Biashara of Tuesday, 16 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

CRDB kufufua kiwanda cha mawese Kigoma

CRDB kufufua kiwanda cha mawese Kigoma CRDB kufufua kiwanda cha mawese Kigoma

BENKI ya CRDB imeonyesha nia ya kutoa Bil 1.2/- kwa ajili ya kufufua mradi wa kiwanda cha Mawese cha Trolle Meesle Tanzania Limited cha kuchakata mafuta ya mawese kilichopo eneo la SIDO mkoani Kigoma.

Serikali imeanza mazungumzo na Benki ili kuona namna ya kukifufua kiwanda hicho.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilolitoa kwa Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda. eneo la sido Kigoma.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma jana na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo yake na wadau mbalimbali wa mradi huo ikiwemo mmiliki wa Kitanzania ambaye amewekeza Mil 450/- na dhamana ya nyumba na shule ili kuanzisha mradi huo.

Amesema katika ufadhili huo benki ya CRDB wameonyesha dhamira ya kukubali kufadhili wakulima ambao wataingia kwenye chama cha ushirika (AMCOS) na kuweza kupata fedha za kuendeleza michikichi yao na kilimo chao.

Bashe amesema mradi huo ambao ulikwama ni wa miaka 6 wa ambao uko chini ya kampuni ya Primaslii, mradi ulifadhiliwa na ubalozi wa Denimark - DANIDA kwa kushirikiana na serikali, ulikamilika 2019, baada mwaka 2019 benki ya TIDB, na DANIDA walikubaliana kuweza kufadhili mradi huo wa kiwanda hicho katika mkoa wa kigoma.

Amefafanua katika uwekezaji wa kiwanda hicho asilimia 70 ya ununuzi wa vifaa za kiwanda zilifadhiliwa na DANIDA, huku asilimia 30 zikitolewa na muekezaji binafsi ambaye ndio kampuni tajwa hapo juu, ambapo waliweka makubaliano ya kisheria katika uwekezaji huo wa Mil 450/- kama dhamana ambayo ni fedha waliyokopa waliweka ya mali zisizohamishika ikiwemo nyumba yake vitu vyake.