Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 17Article 551956

Habari za Biashara of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: MillardAyo

Facebook WhatsApp na Instagram zinaongoza Tanzania

Mitandao ya kijamii Mitandao ya kijamii

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dr. Faustin Ndugulile amesema Tanzania ina Watumiaji wa mitandao ya kijamii milioni 16.5 ambapo Facebook na Whatsapp ndio zinaongoza kwa kuwa na Watumiaji zaidi ya milioni sita wakati Instagram ikiwa na Watumiaji milioni 4.5.

Waziri Ndugulile amesema kwa usajili wa line kwa sasa ni zaidi ya milioni 50 na Watumiaji wa internet wakiwa takribani milioni 30 na wanaofanya miamala ya fedha ni zaidi ya milioni 32.

Dkt. Ndugulile ametoa tathmini hiyo wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kielectroniki wa uratibu na ufuatiliaji wa shughuli za kiserikali utakaosaidia kuweka uwazi na uwajibikaji na kufikisha taarifa kwa umma.