Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 11 21Article 573154

Habari za Biashara of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Hii ndio sababu ya bei za magari kupanda duniani kote

Huenda ikakuchukua muda zaidi kuagiza gari kutoka nje Huenda ikakuchukua muda zaidi kuagiza gari kutoka nje

Viwanda vya kutengeneza magari vilikuwa vikifanya shughuli zao kama kawaida na kuruhusu mtu yeyote kununua gari apendalo zaidi hadi pale palipoibuka janga la COVID-19 duniani kote.

Lakini sasa kutokana na ukosefu wa upatikanaji wa magari duniani kote, watu wanapaswa kusubiri. Na kuna uwezekano huenda ikachuku miezi kadhaa kwao kununua gari.

Hii ni kutokana na kutopatikana kwa magari mapya, hali inayochangia bei za aina mpya za magari kuapanda sana.

Pamoja na hili, bei za magari yaliyotumika pia zinaongezeka. Makampuni makubwa yanazalisha magari kwa kiasi kidogo kwa sababu 'semiconductors', jambo muhimu zaidi kwa uzalishaji wao, haipatikani kwenye soko.

Si hivyo tu, mahitaji ya chipsi pia yanaongezeka kwani makampuni ya teknolojia yanazitumia katika kila kitu kuanzia vifaa vya nyumbani hadi kompyuta, simu za mkononi na vifaa vya michezo ya video.

"Sekta ya semiconductor inajaribu kukidhi mahitaji haya yaliyoongezeka," anasema Susan Golicic, profesa katika Kitivo cha Biashara katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Colorado nchini Marekani.

'Hali ni mbaya sana' Golikic anasema kutokana na kutopatikana kwa chips, watengenezaji wa magari wanalazimika kuamua ni magari gani yatengenezwe na yawekewe rafu.

Watengenezaji wengi wa magari wanatengeneza magari yale tu ambayo yanaingiza mapato mengi kama vile magari ya matumizi ya michezo, malori na magari ya kifahari n.k.

Wataalamu wanasema kuwa "hali hii ni mbaya sana." Profesa wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Harvard Willie Shih ameambia BBC Mundo kwamba ukosefu wa bidhaa hizi umeathiri mlolongo wa utengenezaji unaohusishwa na sekta ya magari. Pamoja na hili, makampuni yanayotengeneza zana ndogo pia yameathirika.

"Pia imekuwa na athari kwenye fursa za ajira zinazotolewa na sekta zote zinazohusiana na utengenezaji wa magari. Hivyo matokeo yanaonekana," anasema Shih.

Japan, nchi yenye watengenezaji magari kama Toyota na Nissan, ilishuhudia kupungua kwa asilimia 46 ya mauzo ya magari nje ikilinganishwa na mwaka jana kutokana na uhaba wa vipuri. Na ukosefu huu unaonesha umuhimu wa sekta ya magari katika uchumi wa Japan.

"Sekta ya utengenezaji wa magari inaaminika kuzalisha asilimia 3 ya Pato la kimataifa," anasema David Menekoff, profesa katika Idara ya Usimamizi wa Uendeshaji na Teknolojia ya Habari ya Chuo Kikuu cha Florida Atlantic University School of Business.

Katika mazungumzo na BBC Mundo, Menekoff anasema kuwa utengenezaji wa magari takribanImilioni nane ulisimama mwaka jana. Na hii ilisababisha hasara ya dola za kimarekani laki mbili kwenye tasnia ya utengenezaji magari.

Bei za magari yaliyotumika zimepanda "Magari nchini Marekani yanauzwa kwa bei ya juu kuliko bei yao ya awali.

Kwa sababu watu wako tayari kulipa zaidi ya bei ya kawaida," anasema Menekoff.

Na kutokana na kutopatikana kwa bidhaa mpya sokoni, mahitaji ya magari yaliyotumika yameongezeka sana.

Kwa sababu ya hii, bei ya wastani ya gari la mitumba huko Amerika imeongezeka hadi zaidi ya dola elfu 25. Susan Golik anasema kuwa wastani wa gharama ya magari inaongezeka kwa dola za Marekani 200 kwa mwezi.

Athari kimataifa Hali iko hivyo hivyo katika sehemu nyingine za dunia pia. Kwa mfano, Mexico ni nchi ya nne kwa uuzaji wa magari nje na mzalishaji wa saba kwa ukubwa duniani.

Inauza nje asilimia 80 ya uzalishaji wake, nchi hii iko mstari wa mbele katika tasnia ya magari huko Amerika Kusini. Na sasa nchi hii pia inakabiliwa na athari za uhaba wa kimataifa katika utengenezaji wa magari.

Anasema, "Kwa sasa mahitaji ni makubwa na magari ni machache.

Na wateja wakati mwingine hulazimika kusubiri kwa muda wa miezi mitano hadi sita kupata gari wanalopenda.

Akizungumzia upungufu huu, Prieto anasema kuwa huu ni upungufu mkubwa sana, unaoonekana wazi katika soko la ajira.

Sekta ya magari hutoa ajira milioni mbili za moja kwa moja na hutoa kazi nyingi zisizo za moja kwa moja ikiwa sehemu na kampuni za huduma zitaongezwa.

Sababu ya ziada imeongezwa kwa uhaba wa magari na hiyo ni kuingia kinyume cha sheria kwa magari yaliyotumika kutoka Amerika.

Magari yaliyotumika yanarejelea yale magari ambayo yako katika hali mbaya na hayapati mnunuzi katika uchumi mkubwa zaidi duniani, lakini kesi za kisheria zinazohusiana nazo zinasubiri kuvuka mpaka.

Athari za kazi na kiuchumi Ingawa magari yanatengenezwa katika maeneo mbalimbali duniani, uzalishaji mwingi unafanywa Marekani na China.

Lakini baadhi ya nchi ndogo kama Slovakia pia hushiriki katika mlolongo wa uzalishaji wa magari.

Idadi ya watu hapa ni milioni 5.6 tu lakini kuna viwanda vya Volkswagen, Piaget na Kia vinavyotengeneza magari milioni moja kila mwaka.

Hili ndilo linaloifanya kuwa nchi ya juu zaidi kwa uzalishaji duniani.

David Menekoff anasema kuwa kwa mtazamo wa kimataifa, ukubwa wa sekta ya magari huleta athari kubwa.

Anasema, "Kampuni inayoajiri watu 100 inaleta athari ya ajira kwa wafanyakazi mia tano" kwa sababu makampuni mengine yanayohusiana na kampuni hii pia yanaajiri watu.

Na wakati kila kipengele kinachohusika katika mlolongo wa utengenezaji wa magari kinapoathirika, pia ina athari mbaya kwa uchumi wa ndani, hasa wakati baadhi ya mitambo imefungwa kwa muda.

Menekoff anasema, "Makadirio yote yanaonesha kuwa upungufu huu unaweza kuendelea hadi mwaka 2022 mpaka mwaka 2023 kabla ya hali ya kawaida ya soko kurejea.