Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 10 07Article 561856

Habari za Biashara of Thursday, 7 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Hizi hapa sababu za shilingi kupanda

Hizi ndo sababu ya Shilingi kupanda Hizi ndo sababu ya Shilingi kupanda

Shilingi ya Tanzania imeendelea kuimarika dhidi ya dola ya Marekani kwa wiki mbili mfululizo sasa, jambo ambalo lina tafsiriwa kama mapinduzi ya kiuchumi hasa kwa wakati huu ambao Serikali inapambana kufikia uchumi wa bluu.

Sababu za kupanda kwa shilingi zimetajwa kuwa ni ongezeko la watalii nchini katika kipindi cha mwezi June hadi Septemba 2021, matumizi makubwa ya shilingi katika manunuzi ya bidhaa za nje, shughuli za uwekezaji pamoja na misaada ambayo imetolewa na wadau wa maendeleo pamoja na IMF.

Wiki mbili zilizopita, Benki Kuu ya Tanzania BOT, ilitangaza kupanda kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola kutoka kuuzwa shilingi 2,310/2,288 hadi 2,284.9 kwa 2307.75.

Hadi kufika jana Oktoba 6, 2021, katika benki ya biashara, Shilingi hii ilikuwa ikiuzwa kwa 2,290/2,320 kutoka kuuzwa 2,313/2,337.5.

Hata hivyo BOT imeendelea kutabiri kuwa shilingi hii itaendelea kuimarika kwa miezi ijayo mbele na kubainisha kuwa ilianza kupanda mwezi Julai, 2021.

Kupanda kwa shilingi ni neema kwa wafanyabiashara, kwani kwasasa watatoa kiasi kidogo kwa ajili ya manunuzi hivyo bei za bidhaa zinatarajiwa kupungua zaidi katika masoko ya ndani nchini.

Bidhaa ambazo zinalengwa kupungua bei zaidi ni pamoja na mafuta,nguo, mafuta ya kupikia na zinginezo.