Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 13Article 557272

Habari za Biashara of Monday, 13 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Hofu ya wakulima wa miti baada ya TANESCO kuanza kutumia nguzo za zege

Ujio wa nguzo mpya TANESCO wawatia hofu wakulima wa mkaratusi Ujio wa nguzo mpya TANESCO wawatia hofu wakulima wa mkaratusi

Wakulima wa Miti ya Mkaratusi mkoani Iringa na Njombe, wameeleza hofu juu ya kupungua kwa soko la miti hiyo kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na serikali kwenye Shirirka la Umeme TANESCO kutoka kutumia nguzo za miti hiyo hadi kutumia nguzo za zege.

Wameeleza hofu yao kufuatia hatua hiyo kwani zao hilo limekuwa likinunuliwa kwa wingi na shirika hilo la Umeme.

Aidha serikali imewatoa hofu wakulima hao kwakuwaambia kuwa zoezi hilo la kubadili nguzo za umeme halimaanishi kusitisha biashara ya miti hiyo.

Miti ya Mikaratusi pia inatumika kutengeneza mafuta ambayo hutumika kama dawa kwa magonjwa kama ya Pumu, na mafuta hayo pia hutumika kwa kupaka kama kilainishi kwenye ngozi zenye matatizo.