Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 06 07Article 541522

Habari za Biashara ya

Chanzo: ippmedia.com

JATU PLC yaanza kuuza hisa zake

JATU PLC yaanza kuuza hisa zake JATU PLC yaanza kuuza hisa zake

Kwa Sasa kampuni hiyo imeshawanufaisha zaidi ya wanachama 32,000 huku ikiwa na lengo la kuwafikia Watanzania zaidi ya milioni 2.

Uzinduzi wa ununuzi  wa hisa hizo umeanza baada ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imeidhinisha waraka wa matarajio wa kampuni ya JATU PLC kwa ajili ya kuuza hisa milioni  1.5 kwa Sh. 500 ulioanza Juni Mosi mpaka Julai 28 mwaka huu.

Uuzaji wa hisa hizo ni katika kutekeleza majukumu yake chini ya sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (sura ya 79 ya sheria za Tanzania) na Mei 31 mwaka huu iliidhinisha waraka wa matarajio wa kampuni ya JATU PLC kwa ajili ya kuuza kwa umma katika soko la awali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ununuzi wa hisa hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa JATU PLC, Peter Gesaya, amesema mpaka sasa kampuni hiyo  wameshafanikisha shughuli  za kilimo  katika maeneo mbalimbali na wameshafikia   hekari 70,000.

“Mpaka sasa tumeshafikia mikoa kumi na tumefanya kilimo cha machungwa, maparachichi, mahindi, alizeti, mpunga, ndizi na mboga, kwa maeneo yote tuliyozalisha unapata hekari 70,000,  tunaamini kupitia kampeni yetu ya buku tano (Sh. 500) inatosha ambayo ni sawa na hisa 10 tutawafikia wananchi wengi zaidi,”amesema Gesaya.

Asema kampuni hiyo imeamua kuingia kwenye soko la hisa ili kupanua kilimo na kuwasaidia wakulima kufanya kilimo chenye tija na kila mwanahisa atalima kulingana na hisa zake.

Amesema JATU  PLC pia imepanga kuboresha  miundombinu ya kilimo kwakutoa pembejeo za kisasa za kilimo pamoja na mbegu.

Join our Newsletter