Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 06 19Article 543412

Habari za Biashara of Saturday, 19 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

KAMPUNI YA SINGAPORE KUWEKEZA UZALISHAJI MCHELE, MAFUTA

KAMPUNI YA SINGAPORE KUWEKEZA UZALISHAJI MCHELE, MAFUTA KAMPUNI YA SINGAPORE KUWEKEZA UZALISHAJI MCHELE, MAFUTA

RAIS Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni za Wilmar International ya Singapore, Kuok Khoon Hong ambaye ameahidi kupanua uwekezaji katika uzalishaji wa mchele na mafuta nchini.

pore hufanya shughuli zake katika nchi za Malaysia na Indonesia.

Katika mazungumzo hayo, Hong ameahidi kuwa kampuni hiyo ipo tayari kupanua uwekezaji wake katika uzalishaji wa mchele na mafuta kwa kuwa mchele wa Tanzania ni bora na wenye soko kubwa duniani na mahitaji ya mafuta ni makubwa ndani ya nchi.

Alisema kampuni hiyo imefurahishwa na dhamira

ya Rais Samia ya kuwavutia zaidi wawekezaji na kwamba tayari imeshawekeza nchini Dola za Marekani milioni 150 katika kiwanda cha kusafisha mafuta ya kupikia, kutengeneza sabuni na tambi ikiwa ni sehemu ya uwekezaji wa takribani Dola za Marekani Bilioni moja barani Afrika.

Kwa sasa kampuni ya Wilmar imekamilisha kujenga kiwanda cha kukoboa mpunga na kufungasha

mchele mkoani Morogoro kitakachokuwa na uwezo wa kukoboa tani 1,000 za mpunga kwa siku na kutoa ajira kwa watu zaidi ya 300.

Akizungumza na mwekezaji huyo, Rais Samia alimpongeza Hong kwa uwekezaji wake chini na amemkaribisha kupanua zaidi uwekezaji huo hususan nkatika uzalishaji na usindikaji wa mafuta ya alizeti, michikichi na kilimo cha umwagiliaji.

Alimueleza kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na kampuni hiyo katika uwekezaji huo na ameagiza Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha na Mipango kuandaa andiko la pamoja na kampuni hiyo litakalowezesha ushirikiano huo hususan katika kupata teknolojia, mbegu na mitaji.

Rais Samia alitoa mwito kwa wawekezaji wengine kuja kuwekeza nchini hasa katika sekta ya kilimo kwa kuwa Tanzania ina eneo kubwa linalofaa kwa kilimo na ambalo halitumiki ipasavyo.

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda, Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dk Ramadhan Dau, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata.