Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 12Article 551239

Habari za Biashara of Thursday, 12 August 2021

Chanzo: Mwananchi

Kampuni 26 za uuzaji mafuta zafungiwa Tanzania hadi zilipe faini ya Milioni 182

Ewura imevichukulia hatua vituo 26 vya mafuta. Ewura imevichukulia hatua vituo 26 vya mafuta.

Mamlaka ya ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (Ewura) imevichukulia hatua vituo 26 vya mafuta kwa kuuza mafuta yasiyo na viwango stahiki vya vinasaba yanayopaswa kutumika Tanzania.

Ewura iliendesha ukaguzi kuanzia Julai 2 hadi Agosti 9, ikabaini vituo hivyo 26 vya ndani na vya kimataifa kuuza mafuta yasiyo na viwango vikiwemo Total, GBP Tanzania Ltd, Lake Oil, Oryx Oil, Oilcom, Camel Oil, na Olympic.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 12, 2021 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura Godfrey Chibulunje amesema kwa kitendo hicho inaonyesha kuwa vituo hivyo vilikiuka sheria na vilikuwa na nia ya kukwepa kodi ya Serikali.

"Hii ina maanisha kuwa wamiliki wa vituo hivyo walichanganya mafuta yao na mafuta ambayo hayajalipiwa kodi wakitaka kukwepa kulipa kodi stahiki. Ewura imevifungia vituo vyote vilivyohusika na kuvilipisha faini kwa mujibu wa kanuni na tayari taarifa zao zimepelekwa TRA," amesema Chinulunje.

Chibulunje amesema ka mujibu wa kanuni vituo hivyo vimetozwa faini ya Sh7 milioni na Ewura kwa kosa hilo lakini pia TRA wamekabidhiwa taarifa zao ili waweze kufanya tathimini ya kodi iliyokwepwa, na kituo kitafunguliwa baada ya kulipa faini na kodi inayodaiwa na TRA.