Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 11 25Article 574066

Habari za Biashara of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Kariakoo yote kufungwa CCTV Camera na mataa

Kariakoo yote kufungwa CCTV Camera Kariakoo yote kufungwa CCTV Camera

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, amesema kuwa bajeti ya Jiji itakayopitishwa kwa mwezi Desemba, watahakikisha wanapambana kuingiza bajeti ya kununua CCTV camera na taa zitakazofungwa katika soko la Kariakoo ili liwe eneo salama zaidi kwa wafanyabiashara.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 25, 2021, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio.

"Lengo letu ni kuifanya Kariakoo watu wafanye kazi saa 24 yaani usiku na mchana,", amesema Meya Kumbilamoto