Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 12Article 551137

Habari za Biashara of Thursday, 12 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Kenya yakusanya Tsh. Bilioni 370 kwenye biadhaa za Tanzania

Bishara kati ya Tanzania na Kenya imezidi kushamiri. Bishara kati ya Tanzania na Kenya imezidi kushamiri.

Usafirishaji wa bidhaa kutoka Tanzania kwenda Kenya umeongezeka kwa kiasi kikubwa, na kwa mara ya kwanza katika miongo kadhaa Ukanda wa Africa Mashariki umeonekana kunufaika na kuashiria ukuaji wa biashara, chini ya Utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Takwimu Mpya zilizotolewa na Benki ya Kenya (CBK) zinaonyesha kuwa uingiaji wa Bidhaa nchini Kenya kutoka Tanzania umekuwa kwa kiwango cha Robo tatu katika kipindi cha miezi sita hadi juni 2021 ukilinganisha na miaka ya nyuma baina ya nchi hizo mbili.

Bidhaa ambazo Kenya huagiza kutoka Tanzania ni pamoja na Mazao ya nafaka, Mbao na mbogamboga na kuongeza mapato katika Mamlaka ya Mapato Kenya (KRA) kwa kiasi cha shilingi Bilioni 370.

Mauzo yanayofanyika kutoka Tanzania yameongezeka kwa asilimia 70.06 ukilinganisha na mauzo ya nje ya nchi za Afrika Mashariki ambayo imeongezeka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka mitano nyuma kwa faida ya shilingi bilioni 21.02 ya biashara.

Takwimu za Benki kuu ya Kenya CBK zimeonyesha uingizwaji bidhaa za Dawa, plastiki, chuma na Nondo kutoka Tanzania umeongezeka kwa asilimia 21.39 na faida ya bilioni 340 kiwango ambacho ni cha juu zaidi kuwahi kutokea tangu mwaka 2016.

Rais Uhuru Kenyatta na Rais Samia mapema mwezi mei waliahidi kuimarisha mahusiano ya kibiashara yaliyo dorora kwa miaka mingi kutokana na kukosekana kwa uingiaji mzuri wa Bidhaa na huduma ndani ya Afrika Mashariki ili kukuza uchumi kwa nchi Sita zilizopo katika ukanda huo.