Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 25Article 553618

Habari za Biashara of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Kenya yasaka Sukari kiasi cha Tanni 210,163 kutoka Comesa

Kenya yasaka Sukari kiasi cha  Tanni 210,163 kutoka Comesa Kenya yasaka Sukari kiasi cha Tanni 210,163 kutoka Comesa

Nchi wanachama wa Comesa jamuhuri ya Eswatini, Zambia na Mauritus zitaisaidia kuingiza sukari Kenya bila ushuru katika Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika( COMESA).Taarifa zinasema sukari hiyo itaingia mwaka huu ili kuzuia kupunguza tatizo la uhaba wa sukari Kenya.

Ugavi wa sukari kutoka mataifa hayo matatu utachangia kwa asilimia 69.5 ya upatikanaji wa sukari Kenya kati ya Tanni 210,163 zinazohitajika kufikia lengo lake la kuagiza sukari Comesa.

Shehena kubwa zaidi ya sukari isiyo na ushuru inatajwa kutoka Eswatini ambayo itaingiza kiasi cha Tani 68,959 ikifuatiwa na Zambia tani 41,152 na Mauritius itaingiza tani 30,036.

Kwa upande wa Afrika mashariki, wafanyabiashara wataruhusiwa kuingiza tani 18,923 za bidhaa hiyo kutoka mataifa ya Uganda, Rwanda tani 4,072 na Burundi tani 0.27.