Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 16Article 551815

Habari za Biashara of Monday, 16 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Kibali cha wekezaji kupatikana kwa siku moja

Mkurugenzi Mkuu wa TIC Maduhu Kazi Mkurugenzi Mkuu wa TIC Maduhu Kazi

Kwa sasa wawekezaji ndani na nje ya nchi wanaweza kupata kibali cha uwekezaji ndani ya siku moja baada ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kutumia mfumo wa kimtandao kukamilisha mchakato huo.

Hatua hiyo ni kubwa kwa kituo cha uwekezaji ukilinganisha na mfumo wa awali ambao ulikuwa ukichukua siku tano hadi saba kupata Kibali cha uwekezaji.

Mkurugenzi Mkuu wa TIC Maduhu Kazi amesema uboreshaji wa mfumo huo umewezekana baada ya wakala wa kukuza uwekezaji kutengeneza mfumo wakisasa wa "Online One Stop Shop System.’ ili kurahisisha mchakato huo.

Mfumo huo ni moja ya jukwaa la Tekinologia ya Habari na Mawasiliano ambalo linawawezesha wawekezaji kupata huduma za TIC kwa haraka mtandaoni.

Kupitia mfumo huo, muwekezaji anaweza kuomba Kibali mahali popote na kwa urahisi na hivyo kupungyuza urasimu na vitendo vya rushwa ambavy vinaweza kujittokeza kati ya muwekezaji na mfanyakazi wa umma.

"Mfumo huo, utaongeza ufanisi katika kutunza nyaraka na kuisadia TIC kutoa huduma kwa muda mfupi." alisema Mauhu.