Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 06 17Article 543163

Habari za Biashara of Thursday, 17 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Kinachokaguliwa na TBS kwenye magari bandarini, 2367 yakutwa na kasoro (+video)

Kinachokaguliwa na TBS kwenye magari bandarini, 2367 yakutwa na kasoro (+video) play videoKinachokaguliwa na TBS kwenye magari bandarini, 2367 yakutwa na kasoro (+video)

Katika zoezi la Ukaguzi wa Magari bandarini, mpaka sasa TBS imeshakagua magari 5,445 na kati ya hayo magari 2367 yalibainika na kasoro zinazotengenezeka.

Hayo yamesemwa na Afisa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania TBS, Diocles Ntamulyango katika ofisi za shirika hilo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi hizo, Bw.Ntamulyango amesema katika magari ambayo yamebainika na kasoro kati ya hayo magari 1567 yamekwisha rekebishwa na kupimwa upya na yamekidhi matakwa ya viwango na yamesharuhusiwa kusajiliwa na TRA.