Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 06 26Article 544306

Habari za Biashara of Saturday, 26 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kituo cha huduma kwa wateja wa TPA chazinduliwa

Kituo cha huduma kwa wateja wa TPA Kituo cha huduma kwa wateja wa TPA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Leonard Chamuhiro amezindua kituo cha huduma kwa wateja cha Mamlaka ya Bandari (TPA).

Akizungumza katika tukio hilo jijini Dar es Salaam leo, Ijumaa, Waziri amesema kuanzishwa kwa kituo hicho ni mwendelezo wa uboreshaji wa huduma za TPA kwa wateja wanaotumia huduma za bandari.

Alisema kituo hicho ambacho kitafanya saa 24 kwa siku kitaisaidia TPA kupata mrejesho kutoka kwa wateja wake na tafiti za kimasoko.

Aliipongeza ushirikiano baina ya TPA na Shirika la Mawasiliano (TTCL) uliozaa kituo hicho ambapo n wateja kupitia mitandao yoyote wataweza kupiga 0800110032 bure kwa lengo la kuwasilisha kero mbalimbali watakazokumbana nazo.

Dk Chamuhiro aliongeza kwa sasa shughuli za upanuzi wa Dar es Salaam zinaendelea vizuri na kwamba uwepo wa kituo hicho cha huduma ni “mwendelezo wa uboreshaji huduma wa bandari.”

Akitoa utangulizi wa kituo hicho, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eric Hamis amesema uzinduzi wa kituo hicho ni mwendelezo wa mamlaka kuboresha huduma zake kiteknolojia kupitia mrejesho kutoka wateja wake.

“Kabla ya kituo hiki, tumekuwa tukiwasiliana na wateja wetu kupitia mrejesho kwenye tovuti zetu na mitandao ya kijamii kama twitter na Instagram,” alieleza.

Alimshukuru Waziri kwa kushiriki tukio hilo huku akimwahidi kuwa kituo cha huduma kwa wateja kitasaidia kuboresha huduma na uhusiano na wadau wa bandari.