Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 10 02Article 560887

Habari za Biashara of Saturday, 2 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Kiwanda cha Dangote chatenga Sh.milioni 648 miradi ya maendeleo Mtwara

Kiwanda cha Dangote chatenga Sh.milioni 648 miradi ya maendeleo Mtwara Kiwanda cha Dangote chatenga Sh.milioni 648 miradi ya maendeleo Mtwara

Kiwanda cha Saruji cha Dangote kimetenga sh milioni 648 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya jamii katika vijiji 13 vya mkoa wa Mtwara.

Hii ni mara ya kwanza kwa Kampuni hii kutenga fedha kwa ajili ya miradi hiyo tangu kuanzishwa kwake 2015.

Miradi ambayo imepewa kipaumbele ni ile iliyo chini ya mipango ya jamii na zile zilizo kwenye malengo endelevu (SDGs) hasa katika nyaja za elimu, afya, huduma za kijamii kama vile maji na usafi wa mazingira.

Akizungumza wakati wa kukabidhi kisima cha maji chenye mita 60 katika kijiji cha Imekua kilichopo Wilaya ya Mtwara vijijini, Afisa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Rachel Singo amesema kuwa kisima hicho kimegharimu jumla ya shilingi milioni 27.

"Tumekuwa tukipokea maombi mengi kutoka kwenye vijiji vilivyo karibu na kiwanda chetu, lakini tumeonelea tuanze kwa kuboresha huduma ya maji, wote tunaelewa kuwa maji ni uhai" amesema.

Ameongeza kusema kuwa, wamejipanga vyema kushirikiana na Serikali katika kutimiza miradi na mikakati iliyopangwa katika vijiji vilivyo karibu na Kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na kupambana na kasi ya maambukizi ya Corona, pamoja na kushiriki kampeni ya upandaji miti katika maeneo hayo.