Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 30Article 554437

Habari za Biashara of Monday, 30 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Kiwanda cha Kuzalisha Nguzo 1500 kwa siku chazinduliwa Njombe

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani

Kiwanda cha Qwihaya chenye uwezo wa kuzalisha nguzo 1500 kwa siku kimezinduliwa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani katika kijiji cha Mtwango kilichopo katika wilaya ya Njombe Mkoani Njombe.

Waziri amesema, Uwepo wa kiwanda hicho utaleta manufaa kwa wakulima wa miti ya nguzo katika mikoa ya Ruvuma na Njombe.

Hadi sasa kiwanda hicho kina idadi ya nguzo 400,000 ambazo zimezalishwa.

Kwa kutambua soko hilo, Waziri amewataka wakazi wa mikoa ya Iringa na Njombe kutumia fursa ya uwepo wa viwanda vya kuzalisha nguzo za umeme kwenye maeneo yao kwa kupanda miti ya kutosha.

Waziri Kalemani amevitaka viwanda vya kuzalisha nguzo za umeme nchini kuzingatia viwango vya ubora ili serikali isiagize nguzo hizo nje ya nchi.