Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 06 05Article 541111

xxxxxxxxxxx of Saturday, 5 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kiwanda cha mbolea Nala kuajiri 3,000

WATANZANIA zaidi ya 3,000 wanatarajia kupata ajira katika kiwanda kipya cha mbolea kitakachojengwa mkoani Dodoma katika eneo la uwekezaji la Nala.

Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Kati Dodoma, Abubakar Mbata alisema Watanzania watapata ajira hizo kutokana na uwekezaji mkubwa wa kampuni ya Itracom kutoka Burundi.

Abubakar alisema, kutokana na viwanda kujengwa katika eneo hilo wakazi walio karibu na eneo la Nala watanufaika kwa kupata huduma mbalimbali ikiwemo kuuza na kununua bidhaa na huduma kwa viwanda na wafanyakazi wake.

Alitaja vipaumbele ambavyo kampuni imevizingatia kabla ya uwekezaji ni pamoja na miundombinu ya umeme na maji kuwa kuhakikisha vinapatikana katika eneo la mradi.

Mhandisi wa Shirika la Umeme (Tanesco) Mkoa wa Dodoma, Tumaini Chonya alisema wamefanya kazi ya kuweka nguzo za umeme pamoja na nyaya kwa asilimia 95 hadi sasa imebaki asilimia tano ambayo itakamilika mapema.

Chonya alisema sambamba na kusambaza nguzo za umeme kwa ajili ya kazi ya uwekezaji, pia wameweka transfoma kwa wananchi walio jirani na barabarani wa eneo la Nala.

Mwekezaji wa eneo hilo mhandisi wa Itracom kutoka Burundi, Msafiri Diedonne alisema," Nilipata wasiwasi wakati nataka kuwekeza lakini miundombinu ya umeme na maji ilikosekana, lakini nashukuru miundombinu hiyo imewekwa, hivyo tunaendelea na uwekezaji na utakapofika wiki ijayo na tutaanza ujenzi wa kiwanda na tutakamilisha miezi tisa ijayo."

Join our Newsletter