Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 23Article 553120

Habari za Biashara of Monday, 23 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Kujiondoa wakopeshaji ujenzi Bomba la Mafuta Hoima - Tanga waongeza gharama dola Bil 5.

Gharama  bomba la mafuta Hoima-Tanga yafikia Dola Bilioni 5 Gharama bomba la mafuta Hoima-Tanga yafikia Dola Bilioni 5

Kujiondoa kwa wakopeshaji kutoka benki kwenye Bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki kumesababisha ongezeko la gharama kwa asilimia 30% sawa na dola bilioni 5 katika mradi huo ambapo itawalazimu wanahisa kuongeza fedha ili kufadhili mradi huo.

Katika mkutano wa Mwaka uliofanyika mwezi may mwaka huu Wanahisa wa kampuni ya mafuta ya Total walithibitishiwa ongezeko hilo la gharama za mafuta ghafi ili kukamilika kwa mradi huo, ambapo dola bilioni 2 utawezeshwa na wanahisa kutoka Equity na wafadhili wa nje.

Ongezeko jipya la gharama kutoka bilioni 3.5 ya awali itawalazimu wafadhili wa mradi huo na wanahisa kukusanya dola bilioni 2.5 na dola bilioni 1 itatoka kwa wakopeshaji wa fedha kutoka equity.

Wanahisa wa Eacop wa bomba la mafuta la Hoima-Tanga pamoja na kampuni ya Total wanamiliki kwa asilimia 62 wakifuatiwa na Kampuni ya mafuta ya Taifa ya Uganda kwa asilimia 15, Kampuni ya Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC asilimia 15 Shirika la Mafuta la Bahari la China kwa asilimia 8.

Benki 10 tayari zimeitahadharisha kampuni ya Eacop hatari za kimazingira ambapo inataraji kuzalisha hewa chafu ya carbon kiasi cha tani 34 kwa kila itakapozalisha mafuta na kuwataka kuzingatia makubaliano ya mkataba wa malengo ya Paris juu ya mabadiliko ya tabia nchi.

Mradi huo ukikamilika kampuni ya Eacop itakuwa moja ya kampuni kubwa inayosafisha mafuta duniani.