Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 10 06Article 561538

Habari za Biashara of Wednesday, 6 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Maagizo ya BOT kwa benki zote nchini

Maagizo ya BOT kwa benki zote nchini Maagizo ya BOT kwa benki zote nchini

Benki Kuu ya Tanzania BOT, imezitaka benki zote za kibiashara nchini kutoa mafunzo ya kiteknolojia kwa watoa huduma wa benki hizo kufuatia mabadiliko ya kidigitali duniani pamoja ili kukidhi mahitaji ya soko.

Haya yamebainishwa na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Fedha kutoka BOT, Jerry Sabi na kusema kuwa mabadiliko ya kiteknolojia na mahitaji mapya ya soko yanalazimisha watumishi wa benki kuwa na ujuzi huo.

"Taasisi za kifedha lazima zitoe mafunzo ya kitaalam ili kuwawezesha wafanyakazi wao kupata ujuzi mpya, ambao utasaidia kuweza kurahisha shughuli za kibenki" Amesema Mkurugenzi huyo.

Ameongeza kusema kutambulishwa kwa bidhaa mpya za huduma za kifedha kama mashine maalumu za kuongea zinazotumiwa na watoa huduma wa kibenki, kadi mpya za malipo, huduma za mtandao za kibenki pamoja na huduma za malipo ya kibenki kwa njia ya mtandao zinawataka watoa huduma za kibenki kuwa na taaluma.