Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 27Article 553987

Habari za Biashara of Friday, 27 August 2021

Chanzo: Mwananchi

Mabasi mwendokasi kufanya safari Mwenge - Morocco

Mabasi mwendokasi sasa kwenda Mwenge Mabasi mwendokasi sasa kwenda Mwenge

Mradi wa mabasi ya mwendokasi jijini Dar es Salaam umeongeza njia na sasa yatafika Mwenge.

Katika njia hiyo iliyoanza kutoa huduma nauli itakuwa ni Sh400 kutoka Shekilango hadi Mwenge.

Hayo yamebainishwa na Msemaji wa wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), Willium Gatambi. Hata hivyo, amesema njia hiyo mpya imeanza kwa majaribio, lakini lengo ni kupunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa jijini la Dar es Salaam.

Mradi huo ulizinduliwa mwaka 2016 ili kupunguza kero za usafiri wa umma hasa kwa wakazi wa pembezoni mwa mji. Ulianza kutoa huduma kwa wananchi waishio Kimara na Mbezi kuelekea mjini, umbali wa kiliomita 21.