Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 27Article 559765

Habari za Biashara of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

'Madini ya Tanzanite yazorota soko la dunia'- Balozi Kairuki

'Madini ya Tanzanite yazorota soko la dunia' 'Madini ya Tanzanite yazorota soko la dunia'

Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki ametaka kuboreshwa kwa matangazo katika madini ya kipekee ya Tanzanite kwenye soko la dunia.

Amesema kuwa licha ya kuwa madini hayo adimu dunia yanayopatikana hapa nchini bado hayafahamiki katika mataifa mengi huku akitolea mfano wa wazi kuwa hayapo kwenye orodha 10 bora ya madini nchini China.

"Kama kutakuwepo na njia sahihi za kuhamasisha na kutangaza , lazima madini ya Tanzanite yashike nafasi za juu katika vito vya thamani ulimwenguni kote" Balozi Kairuki.

Ameongeza kusema kuwa, ili kuongeza ubora wa madini haya, basi ni muhimu kufunga mashine maalum za kusindika madini hayo ili kuongeza thamani katika mauzo, amesema kuwa kwa sasa madini haya yanachakatwa nchini India na kuuzwa New York hivyo hali inayopelekea kutotambulika mahali Madini haya yanapotokea.

Aidha ameshauri mamlaka husika nchini kuhakikisha inakomesha tabia ya uzalishaji bandia wa madini hayo unaofanyika nchini China kisha kuuzwa nchini, kwani vitendo hivyo vinayashushia thamani madini hayo na kupunguza pato la taifa.