Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 05 03Article 536215

Habari za Biashara of Monday, 3 May 2021

Chanzo: ippmedia.com

Mafuta yapo, hakuna haja ya kupandisha bei -Prof. Mkumbo

Mafuta yapo, hakuna haja ya kupandisha bei -Prof. Mkumbo Mafuta yapo, hakuna haja ya kupandisha bei -Prof. Mkumbo

Prof. Mkumbo, amesema hayo leo mara baada ya kutembelea shirika la viwango Tanzania (TBS) jijini Dar es Salaam, amesema mpaka kufikia Tarehe 18 mwezi Mei, meli zingine za mafuta zitakuwa zimeshawasili nchini hivyo hakutakuwa na adha yeyote ya upungufu wa mafuta.

“Hakuna sababu ya msingi kwa wafanyabiashara kupandisha bei ya mafuta kwasababu bidhaa ya mafuta ya kula ipo katika soko letu, hivyo bidhaa ipo ya kutosha na tutadili na wafanyabiashara wanaopandisha bei hovyo hovyo”. Amesema Prof. Mkumbo.

Pamoja na hayo Prof. Mkumbo amewapongeza TBS kwa juhudi wanazozifanya kuhakikisha bidhaa zote zinazoingia kutoka nje na ambazo zinazalishwa hapa nchini zinakuwa na ubora ambao unakubalika.

“Mpaka sasa hatuna rekodi ya bidhaa ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu. hiyo inamaanisha kuna mtu anafanya kazi ya kudhibiti bidhaa ambazo hazifai na mtu huyo anaitwa TBS”. amesema Prof. Mkumbo.Join our Newsletter