Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 11 18Article 572374

Habari za Biashara of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mahakama yaagiza Mgodi wa GGM kuilipa TRA Tsh. Bilioni 6

Mgodi wa GGM  wakwaa kitanzi kuilipa TRA mabilioni Mgodi wa GGM wakwaa kitanzi kuilipa TRA mabilioni

Wakati uongozi wa mgodi wa madini ya dhahabu wa Geita (GGM) ukipambana kujinasua kwenye kitanzi cha kulipa deni la kodi la shilingi bilioni 6, Mahakama ya Rufaa imetoa maamuzi yakuitaka GGM kulipa kiasi hicho kama fidia ambayo ilikwepwa kulipwa kwenye usambazaji wa mafuta kutoka kwa Makandarasi wa mgodi huo.

Uamuzi huo umemaliza vuta ni kuvute ya muda mrefu ya kisheria baina ya GGM na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), sakata hilo limedumu kwa takribani miaka 10 na hii ni baada ya GGM kupinga maamuzi yaliyotolewa na Mahakama Kuu yaliyoitka ilipe kiasi hicho cha fedha kama fidia.

“Mahakama imetenda haki , usambazaji wa mafuta uliofanywa na mkandarasi wao mkuu ulipaswa kulipiwa kodi, na Mahakama hii ya Rufaa imetoa maamuzi haya kwa kufuata kifungu namba 58 cha ushuru ambacho kinaelekeza kuwa TRA wanatakiwa kuchukua kodi hiyo" Alisema mmoja wa Majaji wa Mahakama wa Rufaa.

Mgogoro wa kodi uliibuka zaidi ya muongo mmoja uliopita baada ya mlipa kodi kufanya ukaguzi wa kodi katika masuala ya GGM, na kubaini kuwa kampuni hiyo ilisambaza mafuta kwa kampuni za Geita Power Limited (GPL) na DTP Terrassment, ambazo VAT ilikuwa ikitozwa lakini haikutumwa

Mgogoro huo uliibuka pale ambapo TRA walifanya ukaguzi wa namna GGM inalipa kodi zake na kubaini kuwa mgodi huo ulisambaza mafuta kwa kampuni za Geita Power Limited GPL na DTP Terrassment na kukusanya kodi ambayo hawakuiwasilishwa TRA.

TRA ilifanya mahesabu na kubaini upotevu wa kodi ya shilingi bilioni 6.2 ambayo haikuwasilishwa na GGM.