Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 23Article 559207

Habari za Biashara of Thursday, 23 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mahakama yaokoa milioni 350 za fidia ya Kobil

Mahakama Mahakama

Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali ombi la aliyekuwa mkurugenzi wa kampuni ya mafuta ya Kobil Bwana Fabrice Ezaovi, raia wa Ufaransa kwa kutaka kulipwa fidia ya milioni 350 za Kitanzania baada ya kampuni hiyo kusitisha mkataba wake.

Majaji waliokuwa wakisikiliza rufaa hiyo, Jacobs Mwambegele, Ignas Kitusi na Lucia Kairo walifikia maamuzi hayo mara baada ya kujiridhisha kwa kupokea nyaraka kutoka Tume ya Usuluhishi iliyo thibitisha madai ya bwana Fabrice kuwa hayana mashiko.

Aidha, wamefafanua kuwa maamuzi hayo yamefikiwa kwa kile kinachodaiwa kuwa mlalamikaji alikuwa na nafasi ya kutatua suala hilo la malipo na Uongozi wa kampuni ya Kobil kabla ya kupeleka shauri Mahakamani.

Mlalamikaji anadaiwa kuwasilisha barua ya kuacha kazi kwa uongozi pasipo kutaja sababu za wazi juu ya maamuzi hayo, jambo ambalo ni kinyume na mkataba wa kazi.

Hata hivyo nyaraka za Tume ya usuluhishi zinaonesha kuwa, kampuni ya Kobil ilifanya mchakato wa kusuluhisha suala hilo kabla ya kufika mahakamani, lakini mlalamikaji hakuonesha ushirikiano.