Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 11 16Article 571765

Habari za Biashara of Tuesday, 16 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Majaliwa Atoa Maagizo Wizara ya Viwanda na Biashara

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 16, 2021 amezindua kiwanda cha SIKA kinachotengeneza na kusambaza bidhaa zitumikazo kwenye ujenzi wa majengo, miundombinu pamoja na kwenye viwanda vya utengenezaji (magari, mabasi, lori, reli, mitambo ya nishati ya jua na upepo, facade.

Akiwa kiwandani hapo Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara na hivyo kuwezesha kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Majaliwa pia ameitaka Wizara ya Viwanda na Biashara iendelee na uratibu wa kukutana na Wizara au Taasisi za Serikali na Binafsi nchini ili kuwahamasisha kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.