Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 10 13Article 563071

Habari za Biashara of Wednesday, 13 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Malori yakwama mpakani Kenya-Tanzania siku 30

Malori yakwama mpakani Kenya-Tanzania siku 30 Malori yakwama mpakani Kenya-Tanzania siku 30

Madereva wa maori ya mizigo yaanayosairi kutoka nchini kuelekea Kenya wamelalamikia kusota mpakani kwa takribani mwezi mmoja kwa madai ya kusubiri kufanyiwa uchunguzi.

wamesema tangu wafike mpaka wa Lungalunga nchini Kenya ni muda mrefu umepita wakisubiri ukaguzi huo na hadi sasa hawajafanikiwa kuruhusiwa kuondoka.

Mwakilishi wa madereva hao, Nassoro Ally kutoka Mkoa wa Iringa, amesema kuwa usumbufu huo umesababisha waishiwe fedha za matumizi, jambo ambalo limewaathiri kiuchumi.

“Mpaka sasa hatujapatiwa taarifa yoyote kuhusiana na mkwamo huu, ingawa tukiri kwamba kuna ukaguzi unafanyika kwa malori machache kwa siku tofauti na awali. Kwa siku wanakagua malori zaidi ya 30.

“Sisi wengine, tuna zaidi ya mwezi tupo tu, pesa za kutumia zinatuishia na hatujui hatma yetu mpaka muda huu. Hatujakaguliwa na ukiingia humo ndani hakuna majibu ya kueleweka, yaani hata ukaguzi wenyewe unafanywa kwa kusuasua. Kwa siku wanaweza kukagua malori manne yanavuka kuingia Lungalunga, wengine tunaendea kusota hapa na hatujui hatma yetu.” Amesema dereva huyo.

Nae Ofisa Mfawidhi wa Forodha wa Kituo cha Pamoja cha Horohoro, Mohamed Shamte, amessema malori yaliyoko nje ya lango yakisubiri kuvuka kwenda nchini Kenya, yanasubiri kufanyiwa ukaguzi kutoka upande wa Lungalunga, ambako wamedai wanamabadiliko katika mfumo wa afya