Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 19Article 558313

Habari za Biashara of Sunday, 19 September 2021

Chanzo: millardayo.com

Mapya yaliyopo kwenye iphone 13, maajabu yake, bei yake (video+)

Mapya yaliyopo kwenye iphone 13, maajabu yake, bei yake (video+) play videoMapya yaliyopo kwenye iphone 13, maajabu yake, bei yake (video+)

Kampuni ya Apple ya Marekani inayojihusisha kutengeneza vifaa mbalimbali ikiwemo simu za mkononi aina ya iPhone imeonesha aina mpya ya simu ya iPhone 13 pro na kuonesha baadhi ya vitu vipya vinavyopatikana ndani yake.

Kimuonekano haina utofauti na iPhone 12 pro ila kwenye ufanyaji wa kazi Apple wamesema ina utofauti ikiwemo CPU ambayo Apple wenyewe wamesema ni CPU yenye spidi kuliko nyingine yoyote kuwahi kuwekwa kwenye simu huku camera yake ikija na telephoto 77 mm lens na 3 times optical zoom.

iPhone 13 pro pia imeongezewa kipengele kingine kwenye camera yake kiitwacho CINEMATIC kinacholeta udambwiudambwi wa sanaa ya filamu kwenye simu hii, vilevile kwa mara ya kwanza camera ya simu hii inaweza kuhamisha ‘focus’ automatic wakati wa kurekodi video kutoka kwa Mtu mmoja kwenda kwa mwingine. iPhone 13 Pro na iPhone 13 Pro Max zinaanzia $999 ( Tsh. milioni 2.3) hadi $1099 (Tsh. milioni 2.5) huku ile iPhone 13 pro max yenye terabyte moja ikiuzwa $1,599 (Tsh.milioni 3.7).