Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 11 16Article 571726

Habari za Biashara of Tuesday, 16 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Matumizi ya "Bando za Internet" yalivyoongeza mapato ya Vodacom

Matumizi ya Matumizi ya "Bando za Internet" yalivyoongeza mapato ya Vodacom

Pamoja na kukiri kupata hasara kwenye mapato yake, Ukuaji wa tarakimu mbili katika mapato ya data ya simu uumechochea ongezeko la asilimia tatu la mapato ya jumla ya fedha za nusu mwaka za Vodacom Tanzania.

Vodacom imeripoti kuwa, katika kipindi cha miezi sita hadi kufikia Septemba 30, 2021, mapato ya kampuni yalipanda hadi Sh492.8 bilioni kutoka Sh478.31 bilioni zilizoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2020.

Kampuni hiyo imeonesha kuwa ongezeko la mahitaji ya matumizi ya data nchini yamechangia kwa sehemu kubwa katika kuboresha mapato ya data na hatimaye mapato ya jumla ya huduma.

Kwa mujibu wa matokeo ya kifedha ya muda yaliyotolewa hivi karibuni kwa kipindi hicho mapato ya kampuni ya data kwa njia ya simu yameongezeka hadi Sh107.46 bilioni, kutoka Sh87.37 bilioni katika kipindi kama hicho mwaka 2020.

Ongezeko la asilimia 23 lilikuwa kubwa kuliko vyanzo vingine vya mapato kama vile M-Pesa ambayo ilipanda kwa asilimia 1.1 pekee. Kwa upande mwingine, mapato kutoka kwenye huduma za simu za sauti, zinazoingia na ujumbe zote zilipungua.

Kutokana na hali hiyo, sehemu ya mapato ya huduma za kampuni yameimarika hadi Sh485 bilioni - kutoka Sh474.3 bilioni mwaka 2020 - huku mapato yake yasiyo ya huduma yakipanda hadi Sh7.87 bilioni kutoka Sh4 bilioni katika kipindi hicho.

"Tuliripoti ukuaji wa mapato ya huduma kwa asilimia 2.2 katika kipindi hicho, ukisaidiwa na kuongezeka kwa matumizi ya data ya simu," alisema mkurugenzi mkuu wa Vodacom (MD), Bw Sitholizwe Mdlalose - akiongeza kuwa wateja wa data kwa sasa wanajumuisha asilimia 51.7 ya wateja wote.

Katika matokeo ya fedha, taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji pia ilisema kuwa matumizi ya data kwa mteja yameongezeka na kufikia gigabyte 1.6 kwa mteja kwa mwezi.