Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 10 12Article 562819

Habari za Biashara of Tuesday, 12 October 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mauzo DSE yaongezeka kwa asilimia 168

Mauzo ya DSE yaongezeka kwa asilimia 168 Mauzo ya DSE yaongezeka kwa asilimia 168

Mauzo katika Soko la hisa la Dar es Salaam yanatajwa kuongezeka kwa zadi ya asilimia 168 kwa wiki ziizopita baada ya wawekezaji wa nje kununua hisa kutoka benki za CRDB Plc na NMB Plc.

Mauzo ya wiki katika soko hilo yameongezeka hadi bilioni 1.27 kutoka milioni 510.05 wiki iiyopita.

Uchambuzi wa kina uliofanywa na Vertex International Securities Ltd, umeonesha kuwa benki ya CRDB Plc imeongoza kwa kuuza zaidi ya aslimia 54 ya mauzo yote ya soko.

Ikifuatiwa na NBM Plc iliyouza asilimia 41.07 wakati Jatu Olc ikikamata nafasi ya tatu kwa ukinara wa mauzo katika soko hilo.

Kiasi cha hisa zilizouzwa kimeongezeka kutoka 670,000 kwa wiki zilizopita hadi kufika milioni 3.5 kwa wiki iliyopita.

Wawekezaji katika soko hilo wanatarajia kuwa matokeo haya hayatabadilika kwa wiki zijazo.