Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 11Article 556909

Habari za Biashara of Saturday, 11 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mauzo ya parachichi yapanda

Mauzo ya parachichi yapanda Mauzo ya parachichi yapanda

MAUZO ya parachichi yameongezeka kutoka tani 3,696 mwaka 2015 hadi tani 7,190 mwaka 2019, pia bei ya parachichi imepanda kutoka Sh 1,200,000 kwa tani mwaka 2015 hadi Sh 1,800,000 kwa tani mwaka 2020.

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alitoa takwimu hizo bungeni Dodoma jana wakati akijibu swali la Mbuge wa Viti Maalumu, Dk Pindi Chana (CCM) aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwaunganisha wakulima wa mikoa ya Kusini na wawekezaji wa nje na ndani?

Bashe alifafanua kuwa, mafanikio hayo yamepatikana kupitia ushoroba wa Maendeleo ya Kilimo Tanzania (SAGCOT) ambapo Wizara ya Kilimo imehamasisha na kuwaunganisha wawakezaji wawili; Tanzanice Agrofood Ltd na Olivado Tanzania Ltd, na wakulima wa mikoa ya Njombe na Iringa.

Bashe alisema kampuni hizo zinawahakikishia wakulima soko na kwamba zimekuwa chachu ya kuongezeka kwa uzalishaji, kupanda kwa bei na ubora wa parachichi.

Alisema serikali inatambua umuhimu wa kuwaunganisha wakulima na wawekezaji wa ndani na nje ili kuwa na mfumo endelevu unaotoa faida ya pande zote mbili.

Katika utekelezaji wa mpango huo, alisema serikali kupitia Wizara ya Kilimo imekuwa ikiratibu makubaliano kati ya wanunuzi/wasindikaji na wakulima kupitia kilimo cha mkataba kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa teknolojia, pembejeo pamoja na masoko ya mazao.