Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 27Article 553981

Habari za Biashara of Friday, 27 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Mbaazi laingiza Bilioni 1 Ruvuma

Zao la mbaazi laingiza Bilioni 1 Ruvuma Zao la mbaazi laingiza Bilioni 1 Ruvuma

Chama Kikuu cha Ushirika cha wilaya ya Songea na Namtumbo(Sonamcu Ltd)cha mkoani Ruvuma, kimefanya mnada wa tatu wa zao la mbaazi kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani huku wakulima wakifurahi bei nzuri inayotolewa na wanunuzi.

Meneja wa Sonamcu Juma Mwanga amesema, Sonamcu imefanya minada mitatu na hadi sasa kilo 1,327,513 zimeuzwa na Sh. Bilioni 1,727,765.879 zimelipwa kwa wakulima.

Amesema, katika mnada wa kwanza uliofanyika tarehe 11 Agosti, jumla ya kilo 41,428 zimeuzwa kwa bei ya Sh.1,280 kwa kilo ambazo zimenunuliwa na Kampuni ya Ginning Afrisian ambayo imelipa Sh. 53,027,840.00 na baada ya tozo ya Sh.57 kwa kilo wakulima wameingiziwa jumla ya Sh.50,666,444.00 kwenye akaunti zao.

Amesema, mnada wa pili umefanyika tarehe 18 Agosti na kilo 406,517 zimeuzwa kwa bei ya Sh. 1,320 kwa kilo moja na kufanya fedha zilizoingia kwa mnada huo kufikia Sh.536,602,440.00.

Mwanga amesema,katika mnada huo makampuni matano yalijitokeza kwa ajili ya kutaka kununua mbaazi,hata hivyo makampuni mawili ya Mohamed Enterprises na Lenic Tanzania Ltd ndiyo yaliyoshinda na kupata fursa ya kununua mbaazi zote zilizoingizwa mnadani.