Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 10 08Article 562138

Habari za Biashara of Friday, 8 October 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mfumuko wa bei wafikia asilimia 4.0

Mfumuko wa bei wafikia asilimia 4.0 Mfumuko wa bei wafikia asilimia 4.0

MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi septemba mwaka huu umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.8 kwa mwezi Agosti 2021.

Kuongezeka kwa mfumuko huo kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakuala.

Kaimu Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu, kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ruth Minja, amesema baadhi ya bidhaa za vyakula zilichangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni pamoja na unga wa ngano kwa asilimia 6.8, Nyama ya Ng’ombe kwa asilimia 3.4, Maziwa ya unga kwa asilimia 9.2, mayai kwa asilimia 5.0 na viazi mviringo kwa asilimia 4.7

Kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni pamoja na gesi ya kupikia kwa asilimia 5.7, mkaa Asilimia 3.5 na Huduma ya malazi kwenye nyumba za kulala wageni kwa asilimia 5.7

Vilele mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na Vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia septemba, 2021 umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia agosti 2021.

Mfumuko wa bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa septemba 2021 umeongezeka pia hadi kufikia asilimia 4.1 kutoka asilimia 4.0 ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi agosti 2021

Nako nchini Kenya mfumuko wa Bei kwa mwaka ulioishia septemba 2021 umeongezeka hadi asilimia 6.91 kutoka asilimia 6.57 kwa mwaka ulioishia agosti 2021

Kwa upande wa Uganda mfumuko wa Bei kwa mwaka ulioishia septemba 2021 umeongezeka pia hadi asilimia 2.2 kutoka asilimia 1.9 kwa mwaka ulioishia agosti 2021