Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 11 19Article 572770

Habari za Biashara of Friday, 19 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mgodi mdogo uliotoa dhahabu za Tsh. Bilioni 11.4

Mgodi mdogo uliotoa dhahabu za Tsh. Bilioni 11.4 Mgodi mdogo uliotoa dhahabu za Tsh. Bilioni 11.4

MGODI mpya wa dhahabu wa Mhalo unaochimbwa na wachimbaji wadogo wilayani Kwimba, Mkoa wa Mwanza umetoa dhahabu zenye thamani ya Sh bilioni 11.4 baada ya kuanza uzalishaji hivi karibuni.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Madini, Dotto Biteko alipotembelea mgodi Na Frank Leonard, Mafinga KAMPUNI ya Lush Chanzo inayomilikiwa kwa ubia na wawekezaji kutoka China na Pakistan ipo katika hatua za mwisho kujenga kiwanda cha kwanza nchini cha vifaa vya kutengeneza samani na kufunika kuta.

Kiwanda hicho kitakachojengwa katika eneo la viwanda la Lungemba, Mafinga wilayani Mufindi, mkoani Iringa, kitagharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 15 (Sh bilioni 34) mpaka kukamilika kwake.

Taarifa hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Saad Mtambule ikiwa ni matokeo ya kongamano la uwekezaji katika sekta ya misitu lililofanyika kwa uratibu wa Mkoa wa Iringa, mjini Mafinga huku likishirikisha wadau zaidi ya 400 wa ndani na nje wa sekta hiyo.

Alisema mbali na kutengeneza ajira kwa Watanzania, kiwanda hicho kitaongeza mapato ya wananchi na ya taifa. Mtambule alisema kuanza kuzalishwa kwa vifaa hivyo nchini kunatarajiwa kuleta nafuu kubwa ya bei ya bidhaa hizo zinazoagizwa kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwamo China, Uturuki na Brazil.

“Wilaya ya Mufindi na Mkoa wa Iringa kwa ujumla wake una malighafi za kutosha za kutengeneza bidhaa hizo kutokana na ukubwa wa misitu yake na kwa kufanya hivyo kampuni hiyo na nyingine za kuchakata mazao ya misitu zitakuwa zinatusaidia kutekeleza mwongozo wa kitaifa wa mazao yaliyosindikwa uliozinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizindua kongamano hili,” alisema.

Kwa mujibu wa Mtambule, kujengwa kwa kiwanda hicho kunaongeza idadi ya viwanda vya kuchakata mazao ya misitu kutoka 29 na kufikia 30 ndani ya wilaya hiyo, huku vingine bidhaa mbalimbali ikiwamo nguzo za umeme na samani vikitarajiwa kujengwa. Viwanda hivyo vinatarajiwa kuongezeka baada ya Wizara ya Maliasili na Utalii kupiga marufuku usafirishaji wa malighafi za mazao ya misitu nje ya nchi, katika hatua yake inayolenga kushughulikia changamoto zilizoibuliwa katika kongamano hilo la uwekezaji katika sekta ya misitu nchini.

Akitoa taarifa ya marufuku hiyo inayokwenda sambamba na kusitisha biashara ya utomvu unaozalishwa katika miti ya paini kama malighafi kwa ajili ya kutengenezea gundi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro alionya kwamba watakaokaidi au kukwepa maelekezo hayo ya serikali watachukuliwa hatua kali. Alitoa mwezi mmoja kwa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (Tafori), Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kusaidia kufanya utafiti ili kujua kinachokwamisha viwanda vinavyotumia malighafi hizo kujengwa hapa nchini.

Pamoja na marufuku hiyo, Dk Ndumbaro ameunda timu iliyopewa wiki mbili kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kushughulikia changamoto ya bei ya magogo inayolalamikiwa na wakulima kwa wenye viwanda vya kuchakata mazao ya misitu.

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Happines Seneda alisema watalitumia kongamano hilo kuweka mkakati utakaowezesha wananchi wa Mkoa wa Iringa washiriki vyema katika shughuli ya upandaji miti na biashara ya hewa ukaa. Na Mwandishi Wetu ANANCHI wa Kijiji cha Ndole, Kata ya Kinda, wilayani Mvomero na wa Kijiji cha Ihombwe, Mikumi, Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, wamesema gharama za usajili na ushuru vimewafanya washindwe kufi kisha sokoni mazao ya misitu wanayozalisha kwa njia endelevu.

Vijiji hivyo viwili vipo katika mpango wa matumizi bora ya ardhi, huku vikiendesha usimamizi shirikishi wa misitu na kuzalisha mazao ya misitu kwa njia endelevu. Pia ni miongoni mwa vijiji zaidi ya 30 nchini vilivyojengewa uwezo na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) kwa kushirikiana na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (Mjumita) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC).

Katibu wa Kamati ya Maliasili ya Kijiji cha Ndole, Cosmas Lugwaza alisema juzi kuwa wanatamani kusafirisha mkaa lakini gharama za usajili na tozo mbalimbali zimewafanya washindwe. “Mwaka 2019 wafanyabiashara wa mkaa walikuja kununua kwetu baada ya kuwashawishi wachoma mkaa kupunguza sana bei. Fedha tulizopata pamoja na faini zinazotozwa kwa watu tunaowakamata kwa uhalifu wa mazao ya misitu yetu zimefanya mambo makubwa katika kijiji chetu.”

“Lakini kutokana na Tangazo la Serikali namba 417 kupandisha ushuru, wateja hawafiki huku kwetu lakini na sisi pia tumeshindwa kufikisha mkaa sokoni kwa sababu ya gharama kubwa za tozo na usajili,” alisema Lugwaza. Katibu wa mtandao wa vijiji vyenye mradi wa kuhifadhi misitu kwa kuwezesha biashara endelevu ya mazao ya misitu (CoForEST), Kulangwa Ganda akizungumza katika Kijiji cha Ihombwe, alisema gharama za usajili ni kubwa kwa watu wanaotaka kufanya biashara ya mazao ya misitu.

“Usajili zamani tulikuwa tunalipia Sh 261,000, mwaka jana ukapanda hadi Sh 300,000, lakini mwaka huu umeongezeka tena. Ukilipa hizo Sh 300,000 unaambiwa tena ulipie gharama za upandaji miti Sh 180,000, kwa hiyo jumla inafika Sh 480,000,” alisema na kuongeza: “Hapo hapo ukija kulipia Sh 12,500 ya ushuru wa kijiji unaambiwa tena ulipie asilimia tano ya upandaji miti kwa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS).

Hebu fikiria unataka kusafirisha gunia 200 na hujui soko likoje kwa sababu kuna mkaa unaovunwa kwa njia isiyo endelevu ya bei nafuu utafanya nini?” Aliomba serikali ipunguze tozo hizo kwani ndizo zinawafanya wengi kutumia njia za panya kwenda sokoni na kuikosesha serikali kuu, halmashauri na serikali ya kijiji mapato.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ndole, Adrian Paul aliomba serikali iondoe katazo la vijiji kujipangia tozo ya mazao ya misitu kwani ndio kikwazo kwa wafanyabiashara kufika vijiji vya mbali kama chao. Tangazo la Serikali namba 417 (GN 417) la mwaka 2019 liliondoa mamlaka ya vijiji kujipangia ushuru wa mazao ya misitu na kuweka wa aina moja. Vijiji vya mbali na barabara kuu vilikuwa vikipata wateja kwa kuweka ushuru wa chini, lakini kwa kuweka ushuru wa aina moja wengi hawaendi maeneo hayo. wa Kiliwi uliogunduliwa wiki iliyopita wakati akizungumzia umuhimu wa kuzingatia taratibu za usalama katika kazi hizo ili kuepuka kuporomoka kwa migodi na kuhatarisha maisha kwa wachimbaji.

Utafiti wa kuwapo kwa madini katika mgodi huo ulifanyika mwaka 2018, ambapo sehemu moja ya machimbo hayo imeporomoka hivi karibuni na kuwafukia wachimbaji wadogo tisa ambapo wanane waliokolewa na mmoja bado jitihada za uokozi zinaendelea. Aliwataka wachimbaji katika maeneo mapya ya migodi kufuata maelekezo wanayopewa na wasimamizi wa madini ili wafanye kazi hizo bila ya madhara wakiwa kazini.

“Uhai kwa wachimbaji wa madini ni muhimu kuliko madini, hivyo nataka mamlaka za madini kupitia kwa wasimamizi wenu kuweka juhudi za kuhakikisha Emmanuel Issack anaokolewa akiwa salama,” alisema. Utafiti wa uwapo wa madini ya dhahabu katika Wilaya ya Kwimba umekuwa na mafanikio makubwa baada ya mgodi mwingine wa Kiliwi kugunduliwa hivi karibuni na tayari wachimbaji wadogo wameanza shughuli zao kwa wingi katika eneo hilo. Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoour ameunga mkono juhudi za wachimbaji wadogo katika mgodi huo mpya wa Kiliwi uliopo katika Kata ya Bupamwa kwa kutoa Sh milioni 5 kuwezesha kupatikana kwa huduma ya maji ili waweze kuendesha shughuli zao vizuri.

Aliiomba serikali kusaidia kuweka miundombinu ya kijamii katika sehemu hizo ili kuwezesha wachimbaji kufanya shughuli kwa usalama na kuchangia Pato la Taifa.

Mkuu wa wilaya hiyo, Johari Samizi aliomba Wizara ya Madini kuweka miundombinu ya uchenjuaji wa dhahabu katika eneo hilo pamoja na soko la dhahabu ili kuwapunguzia wachimbaji adha ya kusafiri mbali kwa ajili ya kupata huduma hizo.