Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 10 11Article 562612

Habari za Biashara of Monday, 11 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mgodi wa Barrick wazindua Maabara ya dakika 2

Mgodi wa Barrick wazindua Maabara ya dakika 2 Mgodi wa Barrick wazindua Maabara ya dakika 2

Mgodi wa madini ya dhahabu wa Barrick umezindua maabara mpya itakayotumika kupima madini katika kituo cha madini cha Bulyanhulu.

Uwekezaji huo uliogharimu jumla ya dola 3.7 sawa na shilingi bilioni 8.52 za kitanzania utasaidia kurahisha mchakato wa kuchanganua madini kwa muda wa dakika mbili pekee.

Kulingana na maelezo yaliyotolewa na kampuni hiyo yanaeleza kuwa maabara hiyo ni ya kipekee kwa Afrika nzima na itaendeshwa na mtaalamu kutoka nchini Canada na kuongeza kuwa aina ya maabara hiyo inapatika Austarilia pekee.

Maabara hiyo itarahisha kazi kutoka masaa 12 yaliyokuwa yakitumika kabla katika maabara ya zamani hadi dakika 2 kwa sasa.

"Tumeanzisha aina hii ya maabara nchini Tanzania ambayo ni ya kwanza kwa bara la Afrika, ni sehemu tu ya uwekezaji ambao tumepanga kufanya ili kukuza sekta ya madini nchini" Amesema Mtendaji Mkuu wa Barrick Mark Bristow.

Maabara hiyo ina uwezo wa kuchanganua zaidi ya sampuli 1,000 za madini kwa siku moja, jambo ambalo litaongeza uzalishaji.