Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 06 03Article 540742

Habari za Biashara of Thursday, 3 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Mita mpya za maji "kama king'amuzi maji, yakiisha inaji-lock" (+video)

Mita mpya za maji play videoMita mpya za maji

Serikali kupitia Wizara ya Maji kuanzia mwezi Julai inatarajia kuanza kufunga mita za maji za malipo ya kabla[PRE PAID WATER METERS] ambazo zitakuwa na mfumo wa King’amuzi unaweza ukanunua ukiwa sehemu yoyote duniani

Katibu mkuu Wizara ya Maji mhandisi Antony Sanga amesema utofauti wa mita hizo na mita zingine ni kuwa unaweza ukamgawia jirani uniti za maji kama unavyohamisha salio kwenye simu na akaendelea kupata huduma, vilevile kama unahama nyumba uliyokua ukiishi na kuna uniti zako zimebaki kwenye mita unaweza ukahama nazo pia.

Join our Newsletter