Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 06 08Article 541657

Habari za Biashara of Tuesday, 8 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mkenda ataka mkakati viwanda vya mbolea

Mkenda ataka mkakati viwanda vya mbolea Mkenda ataka mkakati viwanda vya mbolea

WIZARA ya Kilimo imeitaka bodi na menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) iandae mkakati wa kupata mbolea nchini kwa bei nafuu.

Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda ametoa agizo hilo jana alipozungumza kwenye kikao kazi alipoitembelea taasisi hiyo kuona utendaji na upatikanaji wa mbolea. Alikuwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Dar es Salaam.

Aliitaka TFRA pia iandae mkakati wa uanzishwaji viwanda vipya vya mbolea nchini.

Alisema bodi na menejimenti ya TFRA ina jukumu la kuhakikisha uzalishaji mbolea nchini unapewa kipaumbele ikiwamo kuongeza viwanda ili pembejeo hiyo ipatikane kwa urahisi na kwa bei nafuu ili kila mkulima amudu kuinunua.

Alisema bodi na menejimenti ya TFRA wanapaswa kubuni mkakati wa namna bora ya kuongeza uwekezaji nchini ili wakulima wawe na uhakika wa kupata mbolea kwa bei nafuu.

Profesa Mkenda aliwataka watumishi wa TFRA waongeze udhibiti kwenye usimamizi wa ubora wa mbolea hasa kwenye mikoa yenye matumizi makubwa ya mbolea.

Join our Newsletter