Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 30Article 554443

Habari za Biashara of Monday, 30 August 2021

Chanzo: TBC

Mwenge wa Uhuru wamuibua mjasiriamali wa Viatu

Mjasiriamali Muhibu Khatibu Mjasiriamali Muhibu Khatibu

Mwenge wa Uhuru ambao unaendelea na mbio zake mkoani Mtwara, umemuibua mjasiriamali mwenye ulemavu ambaye ana kipaji cha kutengeneza viatu vya ngozi wilayani Tandahimba.

Ukiongozwa na Luteni Josephine Mwambashi ambaye ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka huu, Mwenge huo umetembelea duka la Muhibu Khatibu, na kumpongeza kwa kuwa mbunifu na kuendeleza kipaji chake ambacho kwa sasa kinamuingizia kipato.

Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba imetakiwa kuwahamasisha vijana na kuwapeleka kwa mjasiriamali huyo kwa lengo la kujifunza na kupata ujuzi wa kutengeneza viatu, ili na wao waanzishe miradi yao kwa ajili ya kujiongezea kipato na taifa kwa ujumla.

Khatibu ambaye ni mmoja wa Wanachama wa kikundi cha watu wenye ulemavu cha Muongozo kilichopo wilayani Tandahimba, alipata mkopo kutoka halmashauri ya wilaya hiyo na hivyo kuendeleza kazi yake ya kutengeneza viatu ambapo kwake ni bishara ya kudumu ambayo inamuingizia kipato.