Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 10 14Article 563233

Habari za Biashara of Thursday, 14 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

NARCO yakodisha asilimia 75 ya eneo lake

NARCO yakodisha asilimia 75 ya eneo lake NARCO yakodisha asilimia 75 ya eneo lake

Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) imekodisha maeneo kwa wafugaji, hali iliyochangia kupunguza migogoro baina ya wafugaji hao na watumiaji wengine wa ardhi.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya NARCO Paul Kimiti wakati wa kikao cha mwisho cha bodi hiyo ambayo imemaliza muda wake baada ya kukaa madarakani kwa takribani miaka mitatu.

Amesema bodi hiyo imefanikiwa kusimamia na kuhakikisha wafugaji nchini wanapatiwa maeneo kwa mikataba katika ranchi za Taifa, ili waweze kufuga vizuri na kukuza sekta ya mifugo.

“Tumegawa maeneo ya ranchi takriban asilimia 75 na kubakiza asilimia 25 kwa kuwa Wafugaji nchini wamekuwa na mifugo mingi na wanahitaji maeneo kwa ajili ya kufuga mifugo yao.” amesema Kimiti