Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 05 02Article 535930

Habari za Biashara of Sunday, 2 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

NMB yafunga mfumo wa oksijeni Hospitali ya Chanika

NMB yafunga mfumo wa oksijeni Hospitali ya Chanika NMB yafunga mfumo wa oksijeni Hospitali ya Chanika

BENKI ya NMB kupitia kwa wafanyakazi wake Idara ya Hazina, imekabidhi kiasi cha Sh milioni 3.8 kwa uongozi wa Hospitali ya Chanika iliyopo Ilala Jijini Dar es Salaam, ili kuwezesha ufungaji wa mfumo wa oksijeni katika hospitali hiyo.

Kiasi hicho cha pesa kimechangwa na wafanyakazi hao na kukabidhiwa jana.

Akizungumza wakati wa kukabidhihundi hiyo, Mwakilishi wa Idara ya Hazina (Treasury NMB), Samira Saleh, aliishukuru Ofisi ya Mganga Mkuu kwa ushirikiano uliofanikisha makabidhiano hayo na kwamba wanaamini msaada huo unaenda kuokoa maisha ya mama na mtoto.

Awali akizungumza Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dk Willy Sangu, alisema mfumo wa oksijeni unaofungwa kwa msaada huo,utawasaidia wengi katika wodi mbalimbali, hasa kwenye kipindi hiki cha uwepo wachangamoto za upumuaji.

Wakati huo huo benki hiyo imetoa msaada wa meza 60 na viti 60 kwa Shule za Msingi Mtambani na Mgeule, zilizopoTabata, Ilala jijini Dar es Salaam

Samani hizo zina thamani ya Sh milioni 14, huku ikitoa mabati 170 yenye thamani ya Sh milioni 5 kwa ajili ya shule shikizi Mnauka iliyoko Wilani Newala Mkoani Mtwara.

Akizungumza kabla ya kukabidhi msaadawa Meza na viti, Meneja wa benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard alisemameza na viti hivyo vyenye thamani ya Sh milioni 14, ni sehemu ya mpango wao wa Uwajibikajikwa Jamii (CSR), inayoendeshwa kwa miaka kadhaa sasa kupitia asilimia moja ya faida ya NMB kila mwaka

Join our Newsletter