Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 06 03Article 540682

xxxxxxxxxxx of Thursday, 3 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

NMB yakabidhi mshindi gari la mil 25/-

MKAZI wa Temeke Dar es Salaam, Paulo Swai, aliyeibuka mshindi wa droo ya pili ya Kampeni ya Weka Akiba na Ushinde 'Bonge la Mpango' inayoendeshwa na Benki ya NMB, amekabidhiwa zawadi ya gari dogo la mizigo aina ya Tata Ace 'kirikuu' lenye thamani ya Sh milioni 25.

NMB Bonge la Mpango, iliyoanzishwa Februari mwaka huu, inajumuisha zawadi zenye thamani ya Sh milioni 550, ikilenga kuhamasisha utamaduni chanya wa kuweka akiba kwa wateja, huku ikitumika kurejesha kwa jamii sehemu ya faida ya mwaka uliopita.

Hadi sasa imezalisha washindi zaidi ya 120 waliotwaa zawadi zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 180.

Hafla ya kukabidhi zawadi kwa Swai imefanyika katika Ofisi za NMB Tawi la Tandika.

Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, Benedicto Baragomwa, alimkabidhi mshindi huyo gari lake, akishuhudiwa na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Donatus Richard.

Akizungumza kabla ya kukabidhi Kirikuu hiyo, Baragomwa alibainisha kuwa, NMB Bonge la Mpango imewanufaisha wengi.

Alisema miongoni mwa wateja wao walionufaika, wapo walijishindia pesa taslimu, pikipiki za mizigo aina ya Lifan Cargo, kirikuu.

Alisema zawadi kuu itakuwa gari la kifahari aina ya Toyota Fortuner lenye thamani ya Sh milioni 169.

"Kampeni inaendelea kuelekea 'Grand Finale', na ndio maana tunasisitiza wateja wetu kuendelea kuweka akiba na kufungua akaunti mpya, ili si tu kushindania zawadi, bali kujiwekea akiba kwa maendeleo yao," alisema Baragomwa.

Swai ambaye ndiye mshindi wa gari hilo, aliitaja NMB kama benki ya uhakika linapokuja suala la faida za uwekaji akiba.

Alisema utamaduni chanya alioufanya kupitia benki hiyo umempa gari hilo linalotarajiwa kubadili maisha yake kibiashara na kiuchumi.

"Nilipigiwa simu kuwa nimeshinda gari hii Mei 10, hatimaye leo (jana) nakabidhiwa kweli gari hili. Mwito wangu kwa Watanzania wafanyabiashara na wafanyakazi ni kuitumia NMB ambayo ni benki ya uhakika.”

“Wasio na akaunti wafungue huku, ili kunufaika na zawadi kama hizi,"alisema Swai.

Meneja wa NMB Tawi la Tandika, Ahmed Nassor, alimpongeza mshindi huyo anayehudumiwa na tawi lake, huku akiwataka wateja wake wengine kutumia huduma za benki hiyo ili kujihakikishia moja kati ya zawadi zinazotolewa kupitia NMB Bonge la Mpango.

Join our Newsletter