Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 06 14Article 542539

Habari za Biashara of Monday, 14 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Ngurdoto walipa deni mil 83/- kuokoa mali

Ngurdoto walipa deni mil 83/- kuokoa mali Ngurdoto walipa deni mil 83/- kuokoa mali

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha, Masjala Ndogo ya Kazi, imeamuru wafanyakazi wa Hoteli ya Ngurdoto walipwe malimbikizo ya mishahara kwa kuwa mmiliki, Joan Mrema, ambapo ameingiza Sh milioni 82.69 kwenye akaunti ya Mahakama.

Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Ruth Masam, alisema kiasi hicho cha fedha kimeingizwa kwenye akaunti ya mahakama na Sh milioni 42.69 zililipwa moja kwa moja kwa wafanyakazi, hivyo mwajiri ameshatoa Sh milioni 125 .38.

Mwajiri wa wafanyakazi hao, Beatrice Dallaris aliomba mali za hoteli zilizokuwa zikishikiliwa na dalali wa mahakama zisiuzwe na atawalipa fedha zao kupitia akaunti ya Mahakama.

Mali zilizokuwa zikishikiliwa na Mahakama ni pamoja na kiwanja namba 418 block A kilichopo Usa River, gari namba T847 DPH, mashine tatu za kufulia, mashine za kupasulia mbao, vitanda na magodoro.

Taarifa zinadai kuwa wafanyakazi 93 walikuwa wakidai Sh milioni 129.57.

Wakili wa Serikali anayesimamia shauri hilo, Ofisa Kazi Mkoa wa Arusha, Emmanuel Mweta, alisema kesi hiyo Namba 140 ya Mwaka 2020 inahusu madai ya mishahara kutoka Machi mwaka jana hadi Agosti mwaka jana.

Alisema ulifanyika uhakiki na kubainika kuwa waliostahili kulipwa ni wafanyakazi 84 badala ya 93.

Mahakama hiyo pia ilisikiliza kesi ya pili Namba 140 ya Mwaka 2020 ya madai ya mishahara ya kuanzia Septemba hadi Oktoba mwaka.

Mwajiri aliomba apewe wiki moja alipe wafanyakazi 85 mishahara ya Sh milioni 46.67. Kesi hiyo itasikilizwa Juni 18 mwaka huu.